MCHAKATO WAANZA MJI WA MOSHI KUWA JIJI | BONGOJAMII

MCHAKATO WAANZA MJI WA MOSHI KUWA JIJI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
SERIKALI mkoani Kilimanjaro, imewataka madiwani wa halmashauri za wilaya ya Hai na Moshi kuacha ubinafsi katika upanuzi wa mji wa Moshi kuwa jiji.

Badala yake, madiwani hao wametakiwa kushirikiana kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa mchakato huo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, alitoa agizo hilo jana, wakati wa kikao cha uzinduzi wa kutangazwa kwa upanuzi wa mpaka wa kiutawala na utayarishaji wa mpango kabambe wa mjini wa Moshi.

Alisema baadhi ya madiwani wa halmashauri za wilaya ya Moshi na Hai, wamekuwa na tabia ya kuendekeza ubinafsi katika upanuzi wa mji huo, jambo ambalo limekuwa likisababisha kukwamisha lengo hilo.

Alisema suala la ubinafsi, limekuwa likirudisha nyuma

maendeleo ya wananchi wa wilaya hizo.

“Madiwani wa halmashauri za Moshi na Hai, muwe wazalendo embu acheni tabia za ubinafsi upanuzi wa mji wa Moshi ni la manufaa kwetu wote, ninawataka mshirikiane kwenda kwa wananchi kutoa elimu sahihi juu ya

umuhimu wa mchakato huu”alisema

Alisema na kuongeza wapo baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao

wamewatangazia wananchi eti hawakushirikishwa.

“Ni jambo la kushangaza,wapo wanasiasa wanatoka hapa na kwenda kwa wananchi kupandikiza chuku,uongo na majungu hawakushirikishwa, mchakato huu ulishirikisha viongozi wa

pande zote mbili,” alisema

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Mipango Mji na Ardhi wa Manspaa ya Moshi, Uhuru Mwembe alisema hakuna mwananchi atakaye ondolewa katika eneo lake.

Diwani wa Kata ya Mawenzi,Hawa Mushi, aliziomba baadhi ya taasisi za umma,ikiwamo Wakala wa Barabara Tanroads) na mamlaka za maji kutoa ushirikiano katika

upanuzi huo.

Tayari tangazo la Serikali (GN) namba 219 la kuridhia mapendekezo ya kuongeza mipaka ya utawala ya manispaa ya Moshi kutoka kilomita za mraba 58 hadi 142 ambapo zitamegwa kilomita za mraba 68 halmashauri

ya Moshi Vijijini na kilomita za mraba 16 kutoka Wilaya ya Hai,

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts