MECHI KATI YA MONACO NA BORUSSIA DORTMUND YAHAIRISHWA KUTOKANA NA TISHIO LA MLIPUKO KWENYE GARI | BONGOJAMII

MECHI KATI YA MONACO NA BORUSSIA DORTMUND YAHAIRISHWA KUTOKANA NA TISHIO LA MLIPUKO KWENYE GARI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mchezaji wa Borussia Dortmund Marc Barta

Klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani imethibitisha kwamba mechi kati ya klabu hiyo na Monaco imeahirishwa.

Hii ni baada ya kutokea kwa mlipuko katika basi lililokuwa linasafirisha wachezaji wa klabu hiyo kwenda uwanjani.

Mechi hiyo ya robofainali katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya sasa itachezwa kesho.

Mchezaji wa Dortmund Marc Bartra amejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Klabu hiyo imeandika kwenye Twitter kwamba wachezaji wengine wako salama na kwamba hakukuwa na hatari yoyote ndani au karibu na uwanja.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa vioo vya madirisha ya basi hilo vimevunjika kutokana na mlipuko huo.

Polisi katika jimbo la North-Rhine Westphalia wamefika eneo la tukio na kuanzisha uchunguzi.Mashabiki wa Borussia Dortmund

Maafisa wa polisi wamesema kulitokea milipuko mitatu karibu na eneo la basi hilo.

Dortmund kwa sasa wanashikilia nafasi ya nne katika ligi kuu ya Ujerumani.

Mechi nyingine ya robofainali kati ya Barcelona na Juventus nchini Italia inaendelea.Ujumbe uwanjani kuhusu mlipuko huo

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts