MNYIKA AMTOLEA UVIVU PROF KITILA , ADAI ALIKUA MAMLUKI CHADEMA | BONGOJAMII

MNYIKA AMTOLEA UVIVU PROF KITILA , ADAI ALIKUA MAMLUKI CHADEMA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
MSHAURI wa Chama cha ACT Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo, ametangaza kuachana na siasa na kuwa mtumishi wa umma kwa asilimia 100.


Jana Rais John Magufuli, alitangaza kufanya mabadiliko madogo katika safu ya Makatibu wakuu na kumteua Profesa Mkumbo kushika nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Mbogo Mfutakamba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji.


Mnyika: Imedhihirisha alikuwa mamluki


Mjumbe wa kamati Kuu ya Chadema, John Mnyika, alisema uteuzi wa Profesa Kitila kuwa sehemu ya serikali unadhirisha ilikuwa sahihi kufukuzwa Chadema.


“Huo uteuzi umedhihirisha maamuzi yaliyofanywa na kamati Kuu ya Chadema ya kumfukuza uanachama kutokana na usaliti yalikuwa ni sahihi, kwamba alikuwa anatumika na utawala,” alibainisha Mnyika.


Mwaka 2013, Profesa Kitila, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto na Samson Mwigamba, walifukuzwa Chadema kwa madai ya kukiuka Katiba, sheria na kanuni za chama hicho.


Credit - Nipashe

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts