OMBI LA KUTAKA KUIDHINISHWA MATUMIZI YA BANGI NCHINI KENYA LAUNGWA MKONO | BONGOJAMII

OMBI LA KUTAKA KUIDHINISHWA MATUMIZI YA BANGI NCHINI KENYA LAUNGWA MKONO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Zaidi ya Wakenya 1,400 wanaunga mkono ombi la kutaka kuidhinishwa kwa matumizi ya mmea wa bangi baada anayewasilisha hoja hiyo kuwawasilisha ombi lake mbele ya bunge la seneti.

Iwapo ombi hilo la mtafiti Gwada Ogot litaidhinishwa haitakuwa haramu kupanda ama hata kuuza bangi nchini Kenya.

Gwada Ogot anasema kwamba matumizi ya kiafya pamoja na utumizi wa mmea huo viwandani unaojulikana kwa jina la sayansi kama Cannabis sativa una faida nyingi.

Anasema kuwa matumizi ya mmea huo yataimarisha hali ya uchumi.

Sheria ya Kenya inapiga marufuku utumizi wowote wa bangi na kwamba mtu yeyote atakayepatikana akitumia dawa hiyo atashtakiwa kwa uhalifu.

Ogot anaomba bangi kuondolewa miongoni mwa orodha ya vitu haramu na kutaka sheria mpya kuanzishwa ili kuweka bodi simamizi ya utumizi wa mmea huo.

Ogot pia anataka watu wanaohudumia vifungo kwa kumiliki ,kupanda ,kusafirisha kuuza ama kutumia bangi kuachiliwa huru.

Mtafiti huyo ambaye amekiri kuvuta bangi wakati alipokuwa kijana amesema kuwa mataifa mengi katika bara Ulaya na Asia pamoja na majimbo kadhaa nchini Marekani yamehalalisha utumizi wa Marijuana.

Aliorodhesha Colombia, Mexico, Jamhuri ya Czech, Costa Rica,Ireland ,australia, Jamaica na Ujerumani kama mataifa yaliohalalisha utumizi wa mmea huo.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts