PAMOJA NA WAKENYA KWENDA MAHAKAMANI, MADAKTARI 470 WA TANZANIA WAFURIKA KUSAKA NAFASI | BONGOJAMII

PAMOJA NA WAKENYA KWENDA MAHAKAMANI, MADAKTARI 470 WA TANZANIA WAFURIKA KUSAKA NAFASI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Wakati Mahakama nchini Kenya imezuia kwa muda madaktari kutoka nje kwenda nchini humo kupiga kazi, zaidi 470 wameomba kazi hizo kupitia Wizara ya Afya hapa nchini.


Serikali ya Tanzania imesema mchakato wa kupokea maombi hayo pia utaendelea kwa kuwa haijapokea maelekezo yoyote nchini Kenya.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema bado wanasubiri taarifa rasmi kutoka kwa Serikali ya nchi hiyo.


“Tunasubiri taarifa rasmi kutoka Serikali ya Kenya kwa kuwa wao ndiyo walioleta maombi kwetu. Kama kuna mabadiliko yoyote, naamini watatufahamisha rasmi,” amesema.


Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya madaktari 470 wametuma maombi kati ya nafasi 500 zilizotangazwa za kwenda kufanya kazi nchini humo.


Msemaji wa wizara hiyo, Nsanchiris Mwamaja amesema: “Tumepokea maombi mengi ya kutosha, lakini ikitokea mtu akatuma tunayapokea, hivi karibuni jopo litakaa na kuanza kupitia maombi hayo kabla ya usaili na baadaye kupanga mipango ya namna gani watafika vituo vyao vya kazi.”

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts