SHILOLE AANIKA HADHARANI PETE YAKE YA UCHUMBA | BONGOJAMII

SHILOLE AANIKA HADHARANI PETE YAKE YA UCHUMBA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
STAA wa Filamu za Kibongo, Zuwena Mohammed ameamua kujivisha pete ya uchumba mwenyewe, kitendo ambacho kimezua minong’ono kwa watu wengi wakidai kuwa amevishwa na mtu ambaye hajamuweka wazi.

Akizungumza na Ijumaa, Shilole alisema kuwa aliwahi kuvishwa pete na aliyekuwa mpenzi wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, ikapotea kitatanishi kisha Nuh akaoa mwanamke mwingine hivyo akaona kuliko kidole hicho kibaki tupu, akisitiri.

“Pete ile ya Nuh ilipotea, sijui huwa ni za mashetani? Nimeona ninunue nyingine niivae, hakuna cha mwanaume wala nini, mimi sijaona tatizo kuivaa na huenda ndiyo naiita ndoa,” alisema Shilole.



Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts