TRA YAKUSANYA KODO YA SH TRILIONI 10.87/= NDANI YA MIEZI TISA | BONGOJAMII

TRA YAKUSANYA KODO YA SH TRILIONI 10.87/= NDANI YA MIEZI TISA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imefanikiwa kukusanya kodi ya jumla ya shilingi Trilioni 10.87 katika kipindi cha miezi tisa mwaka wa fedha wa 2016/17 kuanzia Juni mwaka jana hadi Machi mwaka huu.

Makusanyo hayo ni sawa na ukuaji wa makusanyo kwa asilimia 9.99 ukilinganisha na makusanyo ya kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha wa 2015/16 ambapo makusanyo yalikuwa Trilioni 9.88.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, amesema kuwa katika mwezi Machi 2017 mamlaka hiyo imekusanya jumla ya Sh. Trilioni 1.34 ukilinganisha na Trilioni 1.31 ya mwezi Machi mwaka 2016 ambapo ni sawa na ukuaji wa asilimia 2.23.

Aidha alisema kuwa TRA inawashukuru walipa kodi wote ambao wameitikia wito wa kulipa kodi ya serikali kwa hiari kila wakati na hivyo kuiwezesha kutimiza wajibu wake wa kisheria.

“TRA inatoa wito kwa kila mlipa kodi kuwajibika kulipa kwa wakati pamoja na kufichua wale wasiotimiza wajibu wao kikamilifu ili serikali iweze kutimiza malengo yaliyokusudiwa kwa wananchi wake,” alisema.

“Lengo la mwaka la TRA ni kukusanya Trilioni 15.1 ambazo tuna imani kwa kipindi kilichobakia cha Aprili hadi Juni mwaka huu tutazifikisha kutokana na kodi mbalimbali,” aliongeza.

Vilevile alisema kuwa matumizi ya EFD pamoja na zoezi la uhakiki wa TIN katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga, na Pwani linaendelea hivyo wananchi wameombwa kuhakikisha wanatumia mashine za EFD na wale wa mikoa husika wanahakiki TIN zao ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

“TRA inatoa wito kwa mlipa kodi yeyote mwenye malalamiko, maulizo au shida yoyote kuhusiana na masuala ya kodi kuwasiliana na ofisi ya TRA iliyo karibu naye au kupiga simu katika kituo cha Huduma kwa Mteja namba 0800750075/0800780078 au barua pepe huduma@tra.go.tz kwa ajili ya ufafanuzi na kutatuliwa shida yake.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts