Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Bondia Cosmas Cheka
Dar es Salaam. Kukatika kwa umeme kulikatisha pambano la Cosmas Cheka na Haidary Mchajo katika raundi ya tatu kwenye Ukumbi wa CCM Vijana, Kinondoni juzi.
Cheka na Mchajo walipanda ulingoni saa 6:30 usiku wa kuamkia jana, lakini walicheza raundi tatu pekee kabla ya pambano lao kusimama baada ya umeme kukatika katika baadhi ya maeneo Kinondoni.
Mashabiki walilazimika kusubiri kwa dakika kadhaa wakiamini umeme utarejea, lakini hadi saa saba usiku mwamuzi aliamua kumaliza pambano hilo, wakati huo Cheka alikuwa akiongoza kwa pointi.
Mmoja wa wasimamizi wa pambano hilo, Aghapeter Mnazareth alisema pamoja na Cheka kuongoza, lakini matokeo yaliyotolewa ni sare kwa kuwa hawakuwa wamecheza nusu ya raundi walizotakiwa ambazo ni raundi 10.
Katika mapambano ya utangulizi, Kanda Kabongo aliwathibitishia mashabiki kwa kumsambaratisha George Dimoso kwa pointi za majaji 3-0 kwenye uzani wa super middle kg 75.
Pambano hilo lililoibua ushindani wa mabondia wa ngumi na mateke (kick boxing) alikotokea Kabongo na wale wa ‘boxing’ lilivuta hisia za mashabiki wengi huku ‘team’ Dimoso wakiondoka vichwa chini kwa bondia wao kufanya vibaya.
Pambano jingine, Twaha Kiduku alimkung’uta Stam Kessy kwa pointi za majaji 3-0 katika uzani wa welter 66, matokeo sawa na aliyopata Juma Fundi dhidi ya Seleman Mohamed.
Pambano la wanawake kati ya Happy Daudi na Felishe Mashauri lilimalizika kwa Happy kushinda kwa pointi za majaji 3-0.