VIONGOZI WA MATAWI CUF WAMKATAA LIPUMBA | BONGOJAMII

VIONGOZI WA MATAWI CUF WAMKATAA LIPUMBA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Profesa Ibrahim Lipumba ametakiwa kujiweka kando na shughuli za chama hicho kwa kuwa alishajiuzulu nafasi ya uenyekiti.

Kauli hiyo imetolewa leo (Jumatano) na baadhi ya viongozi wa matawi makubwa ya hamasa ya chama cha CUF, mkoa wa Dar es Salaam, wakati wakizungumza na wanahabari jijini hapa.

Miongoni mwa matawi hayo makubwa ambayo yapo zaidi ya 20 ni Chechnya, Osama Bin La den, Kosovo, Mwinyi Mkuu na Saratoga

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mwenyekiti wa CUF, Tawi la Mwinyi Mkuu Magomeni Rashid Abdullah amesema Profesa Lipumba siyo kiongozi wa chama hicho lakini amekuwa na tabia ya kuendesha vikao kinyume cha sheria ambavyo asilimia kubwa vinalenga kukihujumu chama hicho ili kishishinde uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts