WATU 4 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU MWANZA | BONGOJAMII

WATU 4 WASIMAMISHWA KAZI KWA KUJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU MWANZA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Maofisa watendaji wanne wa vijiji pamoja na afisa uvuvi wa kata za Nyanzenda na Bukokwa katika Halmashauri ya wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza Gerald Baraka wamesimamishwa kazi kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kumiliki zana haramu za uvuvi,kukumbatia uvuvi haramu pamoja na kupokea rushwa kutoka kwa wavuvi hao ili kufichua siri za misako dhidi ya uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Buchosa Chrispine Luanda, amewataja maofisa watendaji waliosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kuwa ni Lazaro Batendi wa kijiji cha Kanyala,Emanuel Galula wa kijiji cha Lushamba, Mathew Madebele wa kijiji cha Buhama na Martin Madama wa kijiji cha Nyakasasa.

Nao baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo, wamesema vitendo vya uvuvi haramu ndani ya Ziwa victoria wilayani humo vimeanza kushika kasi upya kufuatia tabia ya baadhi ya watendaji wa vijiji na kata wasio waaminifu,waliotakiwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita uvuvi haramu, kudaiwa kuwa ndio vinara wa kumiliki makokoro ya sangara na nyavu za makila zilizopigwa marufuku na serikali.

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi,mazingira na uchumi katika halmashauri ya wilaya ya Buchosa Charles Mbogo ameiomba Wizara ya kilimo,mifugo na uvuvi kuongeza mapambano dhidi ya uvuvi haramu kwa kuwapatia vitendea kazi na boti za doria ili kudhibiti uvuvi haramu unaotishia kupungua kwa samaki ndani ya ziwa hilo na kuharibu ikolojia yake.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts