MAREKANI YAITISHIA KOREA KASKAZINI | BONGOJAMII

MAREKANI YAITISHIA KOREA KASKAZINI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Ni wazi kuwa Jeshi Marekani limejipanga kwa ulinzi zidi ya vita watakavyo pigana na taifa lolote lakini zaidi kuwatisha mahasimu wao Korea kaskazini.

Idara ya jeshi nchini Marekani kwa mara ya kwanza itajaribu kudungua kombora la masafa marefu lililo na uwezo wa kufyatuliwa kutoka bara moja hadi bara lingine.

Maafisa wa Pentagon wanasema jaribio hilo litafanyika Jumatano, wiki ijayo.

Kumekuwa na wasiwasi mjini Washington kuhusu uboreshaji wa miradi ya kinyuklia na makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini.

Mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani anasema iwapo miradi ya Korea Kaskazini ya kutengeneza makombora haitodhibitiwa, basi taifa hilo lina uwezo wa kutengeneza kombora lenye uwezo wa kufikia Marekani.

Matamshi hayo yanaonyesha wasiwasi wa Marekani kuhusu mpango wa Pyongyang wa kutengeza makombora mbali na mpango wake wa Kinyuklia, ambayo Korea Kaskazini inasema inahitaji kwa ulinzi wake.

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa majaribio hayo yalipangwa mapema na kwamba haijibu kisa chochote.

Pentagon ilitangaza jaribio hilo wakati ambapo Korea kaskazini inatengeza kombora la masafa marefu

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts