MBASHA :"SINA HAMU NA NDOA TENA" | BONGOJAMII

MBASHA :"SINA HAMU NA NDOA TENA"

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
BAADA ya hivi karibuni aliyekuwa mkewe, Flora Mbasha kuolewa na mwanaume mwingine, Mwimbaji wa Injili, Emmanuel Mbasha amefunguka kuwa hana hamu na ndoa hivyo hawezi kuwa na haraka ya kuwa na mke kwa sasa kwani anahoļ¬ a kupata mwanamke msaliti tena.

Akipiga stori na Star Mix, Mbasha alisema kutokana na changamoto kubwa aliyoipata kwenye ndoa, kila mwanamke anayemuona anamuogopa kwa kuwa ameshaumizwa kwa hiyo kwa wakati huu ameelekeza nguvu zake kwenye kazi.

“Unajua ukishaumwa na nyoka hata jani likikugusa unaogopa hivyo sina haraka ya kuoa kwa sasa, bado nipo namuomba Mungu akinionyesha nitaoa na kama haijampendeza basi nitabaki hivihivi,” alisema Mbasha.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts