Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Kuelekea Mwezi mtukufu wa Ramadhan ratiba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itabadilika ili kuwapa Wabunge Uhuru wa kuabudu, Kuswali na Kufuturu kwa wakati.
Mnadhimu Mkuu wa Serikali Bungeni, Jenista Mhagama amewasilisha hoja ya kutengua kanuni za Bunge ili kubadilisha muda wa shughuli za Bunge, hoja ambayo imeungwa mkono na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano hivyo katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Bunge baada ya kuahirishwa asubuhi litarejea saa 10 kamili Alasiri badala ya saa 11 Jioni na litaahirishwa saa 12 kamili Jioni badala ya 1:45 Usiku.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka