KIFO CHA NDESAMBURO CHAMLIZA WAZIRI MKUU | BONGOJAMII

KIFO CHA NDESAMBURO CHAMLIZA WAZIRI MKUU

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapa pole wanachama wa Chadema kwa kuondokewa na kiongozi wa chama hicho, Phillemon Ndesamburo.

Ndesamburo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, amefariki jana ghafla wakati akipata matibabu katika hospitali ya KCMC.

“Alikuwa ni mchapa kazi na hodari na niwape pole wote akiwamo mtoto wa marehemu Ndesamburo, Lucy Owenya na wanachama wa Chadema,” amesema

Waziri Mkuu alituma salamu hizo za rambirambi leo asubuhi hii katika kipindi cha maswali na majibu, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Devotha Minja.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts