KUMBE LOWASA NDIYE ALIYEMPONZA YERIKO NYERERE | BONGOJAMII

KUMBE LOWASA NDIYE ALIYEMPONZA YERIKO NYERERE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mfuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendele (Chadema) Yericko Nyerere amepandishwa Kizimbani na kusomewa mashtaka Matano yanayohusu kusambaza Taarifa za Uoungo kupita mtrandoa wa Facebook.

Mbele ya Hakimu Mkazi Wilbard Mashuari wakili wa Serikali Athaas Elia amemsomea Nyerere mashtaka hayo pamoja na  Kuandika kwenye ukuirasa wake wa Facebook Taarifa za kupotosha.
Wakili Elia alidai kuwa Nyerere siku ya Tarehe 25 Oktoba Mwaka 2015, sehemu isiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam aliandika maneno haya" Mateso ya Ulimboka na Kibanda, Mateso ya kijana wetu wa JKT. Ukikumbuka haya fanya uamuzi sahihi bila ushabiki."

Shtka la Pili ni kuchapisha Taarifa ya uongo ambapo Tarehe 24 Oktoba Mwaka 2015 sehemu isiyojilikana Dar es Salaam, Nyerere aliindika kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa "Taifa la Tanzania kuanzia leo halihitaji AMANI, linahitaji Haki tu" 

Shitaka la Tatu ni kuchapisha taarifa za uongo ambapo mshitakiwa katika ukurasa wake wa Facebook siku ya Tarehr 24 Oktoba mwaka 2015 aliandika kuwa "Siku ya leo mpaka siku ya kuapishwa Lowassa Taifa hili halihitaji AMANI bali Taifa hili linahitaji HAKI tu. Amani ilishatoweka siku nyingi, kilichosalia ni uvumilivu tu. Njia sahihi ya kulitibu Taifa hili ni kwa dola dharimu kutenda HAKI hata kama itawauma. Uchaguzi huu ni vita, anaedhani ni demokrasia apimwe akili. Hii ni vita kati ya UMMA na DOLA, ni vita kati ya wema na ubaya, ni vita kati ya shibe na njaa, ni vita kati ya masikini na matajiri"

Shitaka la la nne lilomkabili Nyerere ni kuchapisha taarifa za uongo ambapo tarehe 24 Agosti mwaka 2015 sehemu isiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam, kyupitia mtandao wa Facebook aliandika kuwa "Mipango ya hujuma ya JK toka Ngordoto Arusha muda huu. Kikwete yuko Ngordoto arusha na wakuu wote wa mikoa na Wilaya Tanzania nzima, Pia wakuu wa vyombo vya dola na wanadimu mbalimbali Wakuu wa Mikoa wanaelezwa kwamba kuwa NEC kwa kushirikiana na CCM tayari wameshatengeneza kura bandia kwa kutumia mfumo wa kalamu za kichina, pia wanaamuliwa kuhakikisha wanahujumu kampeni za UKAWA kwa kutumia vyombo vya dola"

Pia wanaagizwa kuhakikisha kamatakamata ya vijana bodaboda wiki moja kabla ya uchaguzi, na zaidi ni wakuu hao wa mikoa wanaagizwa wakawaagize ma DC kote nchini kuhakikisha wanalinda maslahi ya CCM popote walipo siku ya uchaguzi.
Shitaka la Mwisho ni la kuchapisha Taarifa za uongo pia ambapo mtuhumiwa aliiandika kwenye mitandao ya kijamii siku ya Terehe 3 Septemba mwaka 2015 aliandika kuwa HSBC BANK, NORTH LONDON BRANCH. Ccm has deposited 1.5 Pound Million fraudulently in favour of Dr Wilbroad Slaa Through his fuience Josephine Mushumbusi being Curruption from ccm to win Tanzania General Election 2015.
mshtakiwa amekana mashtaka yote na kudhaminiwa kwa shilingi 10 Milioni.
kesi hiyo itatajwa tena tarehe 5 mwezi juni mwaka huu.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts