ZITTO KABWE ABAKI NJIA PANDA BAADA YA UTEUZI WA ANNA MGWHIRA | BONGOJAMII

ZITTO KABWE ABAKI NJIA PANDA BAADA YA UTEUZI WA ANNA MGWHIRA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD


Kiongozi wa Chama Cha Act-Wazalendo hajajua cha kujibu kuhusu suala la uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama hicho Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Zitto amesema kuwa Chama hicho kitatoa tamko baada ya Mwenyekiti huyo kurejea nchini kutoka nje ya nchi alipokwenda .

"Nimekuwa naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka katika vyombo vya Habari. Mwenyekiti yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za masaa bado hatujawasiliana nae

Aliyeteuliwa ni Mwenyekiti wa Chama Taifa, sio mshauri au mwanachama tu. Ni mmoja wa viongozi wa juu wa Chama chetu. Uteuzi wake unahitaji kikao cha Kamati Kuu ya Chama kukaa na kujadili. Nitaweza kutoa Taarifa baada ya vikao vya Kamati Kuu ya Chama. Kwa sasa umma usubiri vikao Kwa mujibu wa Katiba ya Chama chetu" amesema Zitto.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts