JOYCE KIRIA AWAKALIA KOONI WAKAA UCHI MTANDAONI | BONGOJAMII

JOYCE KIRIA AWAKALIA KOONI WAKAA UCHI MTANDAONI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
KUTOKANA na matukio ya baadhi ya wanawake kujianika uchi mitandaoni kushika kasi, Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria ameibuka na kuwapa somo kwamba, waachane na kujiuza, kisa njaa na kama wanapenda umodo, basi wafuate kanuni na taratibu za kimaadili na si kutumia njia hiyo.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Joyce alisema kuwa, anashangazwa na wanawake wanaojianika uchi mitandaoni hivyo kuwataka waache kwani baadaye watajutia baada ya kupata madhara makubwa.

“Mimi mwenyewe maisha ya kutegemea wanaume kwa kutafuta fedha nimeyaishi na yalinitesa sana maana unajikuta unajichosha na kujiingiza kwenye mambo ya hatari,” alisema Joyce. Joyce alimalizia kwa kusema kuwa, mwisho aliamua kutumia akili na hadi sasa ni mjasiriamali na fedha anayoipata anaifurahia kwani anaamini ni jasho lake.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts