MAKAMPUNI YATAKAYOSHINDWA KUJIUNGA SOKO LA HISA KUKIONA CHAMOTO | BONGOJAMII

MAKAMPUNI YATAKAYOSHINDWA KUJIUNGA SOKO LA HISA KUKIONA CHAMOTO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Serikali imesema haitasita kuyafuta makampuni ya madini pamoja na ya simu ambayo yanaendelea kukaidi agizo la kujiunga katika soko la hisa la Dar es Salaam

Waziri wa Fedha na Mipango Dr.Philip Mpango amesema hayo jijini DSM wakati wa zoezi la kuorodhesha kampuni ya Vodacom katika soko la hisa la dsm na hisa kuanza kuuzwa ndani ya soko hilo.

Dr.Mpango amesema serikali haipo tayari kuona maagizo yake yanapuuzwa hivyo ameyataka makampuni hayo ya simu na ya madini kutekeleza maagizo hayo.

Naye Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya simu ya Vodacom Ian Ferao amesema kuanza kuorodheshwa huko katika soko la hisa la Dar es Salaam sambamba na hisa kuanza kuuzwa kutaifanya Vodacom kuwa moja Kati ya makampuni yanayojiendesha kisasa zaidi.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts