Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea Pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa Pikipiki ya TONGBA ya China.
Hatua hiyo inakuja baada ya RC Makonda kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha ombi la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwaajili ya kuongoza Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha Wagonjwa waliozidiwa Hospitalini ambapo kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa kutoa Pikipiki hizo.
Makonda amesema lengo lake ni kuboresha Mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata *Baiskeli 500, Pikipiki za kawaida 200 Computer 100, Pikipiki za Trafic 10 na kufanya maboresho ya Magari ya Jeshi hilo yaliyokuwa yameharibika.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka