MASHABIKI WA SIMBA WAMNUNULIA MAJI MASAU BWIRE KUMPOZA MACHUNGU | BONGOJAMII

MASHABIKI WA SIMBA WAMNUNULIA MAJI MASAU BWIRE KUMPOZA MACHUNGU

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Pamoja na majigambo yake, mashabiki wa Simba waliamua kumnunulia maji Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ili kumpoza machungu.

Simba imeitwanga Ruvu Shooting kwa mabao 7-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara ikiwa ni siku chache baada ya mwalimu huyo kitaaluma ambaye ni msemaji wa timu hiyo ya jeshi kusema Simba ni toy au mwanasesere.

Mashabiki hao waliamua kumnunulia Masau maji ya kunywa na kumpelekea kwenye gari la wachezaji wa timu ya Ruvu.

Kabla ya hapo, wengi waliamua kupiga naye picha wakimvisha kofia za Simba na wengine wakimshangilia.

Muda wote baada ya mchezo huo kwenye Uwanja wa Uhuru, Masau alionekana mtulivu na asiye na makuu

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts