MASOGANGE AKUTWA NA KESI YA KUJIBU | BONGOJAMII

MASOGANGE AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Msanii Agnes Gerald maarufu Masogange, anayetuhumiwa kutumia dawa za kulevya amekutwa na kesi ya kujibu.


Uamuzi huo umetolewa leo Agosti 31, na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Constatine Kakula, kufunga ushahidi wao kwa mashahidi watatu.


Mashahidi wa upande wa Jamhuri waliotoa ushahidi kwenye kesi hiyo ni Mkemia Elias Mulima kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye alipima sampuli ya mkojo na maofisa wawili wa polisi ambao walimpeleka Masogange kwa mkemia.


Baada ya kutolewa kwa uamuzi huo, Masogange ambaye anatetewa na Wakili Reuben Simwanza, alidai atajitetea kwa njia ya kiapo na atakuwa na mashahidi watatu.


Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12, mwaka huu, kwa ajili ya utetezi na kusema dhamana ya mshitakiwa inaendelea.


Masogange anadaiwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo yasiyofahamika Dar es Salaam, alitumia dawa aina ya heroin na Oxazepam.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts