Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, amemsimamisha kazi Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Bw. Denis Kitali kwa kukiuka makubaliano kati ya Idara na Ofisi yake kuhusu namna bora ya kuuza viwanja 380 katika eneo la Msijute
Akitangaza uamuzi huo wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani lililokutana kujibu hoja za Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, CAG, Mkuu huyo wa Mkoa, amesema, licha ya kusimamishwa kazi, hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha, Bi. Dendego amewaagiza baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo walioshirikiana na wanasiasa kutafuna fedha zilizotengwa kwa ajili ya uuzwaji wa viwanja hivyo kuzirudisha fedha hizo mara moja.
"Wapo viongozi waliokula pesa na ushahidi ninao Hakuna wa kupewa kiwanja kiholela hapa. Najua wao waliotafuna pesa hizo na saizi tunazungushana hapa Watapike pesa za watu walizokula" Bi Halima Dendego.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka