Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Rais wa Misri Abdel Fattah El sis anatarajiwa kuingia Nchini (Kesho) siku ya Jumatatu tarehe 14/08/2017 kwa ajili ya ziara ya siku mbili ambapo ataongozana na ujumbe wake na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli.
Kutokana na ugeni huo mzito Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji la Dar es salaam ikiwemo wenye Hotel,Magari na Migahawa kuchangamkia fursa ya ugeni huo katika kufanya biashara ili kujipatia kipato na kukuza Biashara zao.
Makonda amewataka wakazi wa Dar es salaam kuonyesha ukarimu tangu Rais atakapowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere hadi hapo atakaporejea nchini Misri siku ya Jumanne.
Ugeni huu ni matunda ya uwezo wa Rais Magufuli katika kujenga mahusiano mazuri baina ya Tanzania na Mataifa mbalimbali ulimwenguni.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka