Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
AMISSI TAMBWE.
HUKU ikijiandaa kucheza kwa tahadhari katika mechi ya kesho ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Lipuli FC kutoka Iringa, mshambuliaji wa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Amissi Tambwe amerejea kwenye kikosi tayari kuisaidia timu yake kusaka pointi tatu muhimu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga Mzambia, George Lwandamina, alisema kuwa tahadhari hiyo inatokana na kutowafahamu Lipuli ambao wamepanda daraja msimu huu, lakini kikubwa amejiandaa kukabiliana na ushindani.
Lwandamina alisema kuwa akili na mawazo yao yote sasa yamehamia kwenye mechi hiyo huku akisema matokeo ya mchezo wa Ngao ya Jamii ambao walifungwa na mahasimu wao Simba penalti 5-4 sasa ni historia.
"Akili zetu zimehamia kwenye ligi, tulifanya mazoezi kwa ajili ya msimu mpya na haikuwa Simba peke yake, ila kila mechi kwetu ni muhimu kwa sababu safari ya kutetea ubingwa ndiyo imeanza," alisema Lwandamina.
Naye meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema kuwa Tambwe ambaye hakucheza mechi ya Ngao ya Jamii kutokana na kuumia goti amepona na kesho atacheza mechi hiyo ya kwanza ya ligi.
Saleh aliwataja wachezaji ambao hawatacheza kesho ni pamoja na Benno Kakolanya, Geofrey Mwashiuya na Obrey Chirwa ambaye amesimamishwa mpaka pale adhabu yake kamili itakapojulikana.
"Kesho (leo) asubuho tutafanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo ya kwanza, mwalimu haifahamu Lipuli lakini hii haitufanyi tuwe na wasiwasi, tutacheza kwa umakini kwa sababu siku hizi hakuna timu ndogo," alisema meneja huyo.
Mmoja wa wachezaji tegemeo wa Lipuli ni Omega Seme ambaye aliwahi kuichezea Yanga.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka