WAMACHINGA WAMWEKA PABAYA MKUU WA WILAYA | BONGOJAMII

WAMACHINGA WAMWEKA PABAYA MKUU WA WILAYA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
MKUU WA WILAYA YA MOMBA MKOANI SONGWE, JUMA ILANDA.

KITENDO cha Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Juma Ilanda, kuwafukuza wamachinga kwa kutumia nguvu ya Jeshi la Polisi, kimemfanya madiwani watangaze kutoshirikiana naye .

Madiwani waliochukua hatua hiyo dhidi ya DC huyo ni wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Ally Mwafongo (Chadema), alitangaza kwamba madiwani hawatampa ushirikiano Ilanda, kutokana na kitendo chake cha kuwasumbua na kuwabughudhi wananchi hasa wamachinga.

Ilando anashutumiwa kuamuru wafanyabiashara hao waondolewe kwenye maeneo yao ya biashara bila kufuata utaratibu wala kushirikisha uongozi wa halmashauri.

Mwafongo alitangaza uamuzi huo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma.

Alisema Baraza Madiwani la Mji wa Tunduma na wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa inayoongozwa na chama chake, hawako tayari kufanya kazi naye kwa kuwa aliendesha kazi ya Jeshi la Polisi kuwatawanya wamachinga na kupigwa mabomu bila madiwani kushirikishwa kama wawakilishi wa wawananchi.

Mwafongo alisema anashangazwa na hatua ya DC huyo kuwatimua wamachinga kinyume cha agizo la Rais John Magufuli, ambaye mwaka jana aliziagiza halmashauri zote nchini zisiwabugudhi wafanyabiashara wadogo, badala yake ziwatafutie maeneo ya kufanyia biashara kwanza.

“Namshangaa huyu DC kwa uamuzi wa kutumia askari kupiga mabomu ya kuwatimua wamachinga wakati anajua utaratibu wa kuwaondoa unafanywa kwa kupitia vikao vya baraza la madiwani, amewaondoa bila kufuata utaratibu na kibaya zaidi wanawapiga mabomu,” alisema Mwafongo.

Alisema diwani yeyote au kiongozi wa Serikali ya Mtaa atakayetoa ushirikiano kwa DC huyo aatachukuliwa hatua za kinidhamu.

Kwa upande wake DC Ilando alikiri kusimamia zoezi hilo na kwamba ofisi yake itaendelea kuwaondoa wote wanafanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Akizungumzia juu ya baraza la madiwani kusitisha ushirikiano na ofisi yake, Ilando alisema kwake suala hilo halimpi shida na pia halimzuii kutekeleza majukumu yake kama ya kazi.

“Mimi nitaendelea kuwaondoa wote ambao watakuwa wakifanya kazi katika maeneo yasiyoruhusiwa na hata suala ya madiwani kutotoa ushirikianao kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya halina tatizo na wala hainizuii kutekeleza majukumu yangu,” alisema Ilando.

Hivi mitihani waliopigiwa simu na matapeli wanaojifanya kuwa ni watumishi wa taasisi hii na wanauwezo wa kubadili matokeo," alisema Dk. Lukumay.

"Tunapenda kuwatahadharisha wanafunzi wote na umma kwa ujumla siyo sisi bali ni matapeli.

karibuni, DC huyo alitumia Jeshi la Polisi kutekeleza operasheni ya kuwaondoa wamachinga katika maeneo mbalimbali katika Mji wa Tunduma, hali iliyozua sintofahamu kwa wananchi na madiwani wa Mji huo.


Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts