CCM YAMPONGEZA MBUNGE WAO ALIYEKODI NDEGE YA KUMSAFIRISHA TUNDU LISSU | BONGOJAMII

CCM YAMPONGEZA MBUNGE WAO ALIYEKODI NDEGE YA KUMSAFIRISHA TUNDU LISSU

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza mwanachama wake aliyejitolea kudhamini ndege iliyomsafirisha Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kwenda jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya matibabu.


Katika taarifa hiyo, imesema kuwa wamechukua hatua hiyo ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Salim Hassan Turky kwa kuonyesha upendo, utu na mshikamano na kuweka kando tofauti za kisiasa.


“Kwa dhati kabisa tunampongeza mwanachama wetu na mbunge wa Jimbo la Mpendae, kwa kuonyesha utu na kuweka kando itikadi za kivyama kumsaidia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu,” amesema Polepole kupitia taarifa hiyo


Hata hivyo, Polepole ameongeza kuwa wameamua kumpongeza mbunge huyo kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu, kwani katika matatizo ni vyema itikadi za kisiasa zikawekwa pembeni ili kuweza kutatua kile ambacho kinakuwa kinawakabili.


Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts