CHADEMA WAITIKA WITO WA POLISI | BONGOJAMII

CHADEMA WAITIKA WITO WA POLISI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Dkt. Vincent Mashinji,
Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo Septemba 11, 2017 kimeitikia wito wa jeshi la polisi kwa baadhi ya viongozi wake wakuu kufika makao Makuu ya jeshi hilo la Polisi jijini Dar es Salaam kufuatia sakata la Tundu Lissu.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene imesema Dk Mashinji ameambatana na wasaidizi wake kutoka makao makuu ya chama hicho.

“Katibu mkuu amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam, kuitikia wito wa Polisi uliotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, kuwa anatakiwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)” amesema.

Awali, leo Jumatatu Dk Mashinji alisema hawezi kwenda kuripoti kwa kuwa hakuambiwa siku maalumu ya kwenda.

Kamanda Muroto amemtaka Dk Mashinji afike ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Dodoma au ofisi kama hiyo iliyopo Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ili kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

“Nina taarifa za kuitwa Polisi, lakini haziko ‘specific’. Ni wakati wowote naweza kwenda? na hawajasema nikaripoti wapi. Kwa hiyo, wakinihitaji watakuja kuniambia,” alisema Dk Mashinji leo asubuhi.

Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mchana alipokuwa akielekea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.

Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, Kenya

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts