CHADEMA YAITAKA KATIBA YA KENYA | BONGOJAMII

CHADEMA YAITAKA KATIBA YA KENYA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemuomba Rais John Magufuli kurejesha mchakato wa Katiba mpya uwanjani ili uweze kubadilisha baadhi ya vipengele vilivyomo katika Katiba hiyo ambayo inatumika hivi sasa.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Itifaki, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema kupitia ukurasa wao wa facebook baada ya Mahakama ya Juu ya Kenya kuiwekea nchi hiyo historia ya kwanza kwa kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu uliyofanyika Agosti 8, 2015 nchini humo na hatimaye kurudiwa upya ndani ya siku 60 kutokea sasa.

"Ni wakati muafaka sasa Tanzania tukarejea katika mchakato wa kupata Katiba Mpya na yenye kuweka taasisi imara. Rais John Magufuli amdhibitishe Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania kwani hadi sasa amekaa muda mrefu akikaimu tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo", alisema Mrema.

Aidha, Mrema amewataka watanzania waamke kwa pamoja ili waweze kudai Katiba Mpya ambayo anaamini itaweza kuleta uchaguzi uliokuwa huru na haki nchini.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts