MAGARI 26 YALIYOKARABATIWA YAZIDI KUMPA KIKI PAUL MAKONDA | BONGOJAMII

MAGARI 26 YALIYOKARABATIWA YAZIDI KUMPA KIKI PAUL MAKONDA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo September 15, 2017 amefanya ziara Kilimanjaro kukagua ukrabati wa magari mabovu 26 ya Jeshi la Polisi DSM ambayo awali yalikaa kwa muda usiopungua miaka mitano bila kufanya kazi.

Magari hayo sasa yamekamilika na yanatembea na katika wiki mbili zijazo yatakabidhiwa rasmi kwa ajili ya kuongeza na kuboresha ulinzi katika Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na kukarabatiwa kwa mfumo kisasa tofauti na awali.

RC Makonda ameridhika na muonekano wa sasa wa magari hayo ambayo yatarejea barabarani huku akifanikiwa kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingetumika kununua magari mengine.

”Wako baadhi ya wananchi walibeza hili wazo langu la kuyakarabati magari haya kwa kiwango cha Kimataifa, lakini sasa nafurahi kuona ndoto yangu imekuwa kweli. Ni jambo jema kwa Mkoa wetu.” – RC Makonda.





Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts