MANARA NA JAFAR IDD MAGANGA WATUPIANA VIJEMBE | BONGOJAMII

MANARA NA JAFAR IDD MAGANGA WATUPIANA VIJEMBE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Ikiwa imebakia siku moja vumbi kutimuka katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa timu ya Simba na Azam FC katika uwanja wa Chamazi, wasemaji wa klabu hizo wameanza kushika masharti kwa kila mmoja kuweka ahadi ya kumchapa mwenzake.

Hayo yameibuka baada ya kufanya mazungumzo ya pamoja leo Jijini Dar es Salaam katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambako pia alihudhuria Afisa usalama wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) anayetambulika na Shirkisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) Inspekta Hasheem Abdallah ili kuweza kuweka mambo sawa katika mtanange huo.

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema licha ya kuwepo changamoto ya ushidani katika mechi hiyo lakini anaimani kubwa kuwa wataweza kutoa burudani kwa wapenda soka ndani ya dakika 90 zote za mchezo huo.

"Najua kutakuwepo na changamoto kubwa ya ushindani katika mechi yetu ya Jumamosi dhidi ya Azam FC lakini niwahakikishie mashabiki wa Simba kuwa kutakuwa na burudani ya aina yake kwa sababu tumewachukua wachezaji wao wanne. Sasa watacheza wakiwaonyesha walikosea wapi kuwaacha wachezaji hao", amesema Manara.

Naye Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddy Maganga amesema watahakikisha wanatumia vizuri kiwanja chao ili kuweza kuvuna pointi tatu.

"Sisi tunaamini mchezo utakuwa na changamoto kubwa ukizingatia ndugu zetu Simba wamefanya usajili mzuri ambao wao na mashabiki zao wanaamini ni timu nzuri lakini sisi tunasema tumejiandaa vizuri na tumeshacheza mechi za ndani na nje nchi za kujiweka sawa. kwa hiyo maandalizi yapo vizuri na siyo kwa ajili ya Simba SC peke yake ni maandalizi kwa ajili ya msimu mzima wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara", amesema Jaffar.

Kwa upande wake, Ispekta Hasheem amewataka mashabiki wa soka kukata tiketi mapema pamoja na kuwahi kufika uwanjani ili kuweza kuondokana na usumbufu ambao unaweza kusababisha vurugu uwanjani hapo.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts