MANJI APATA PIGO ZITO, SERIKALI YAMNYANG'ANYA SHAMBA LAKE | BONGOJAMII

MANJI APATA PIGO ZITO, SERIKALI YAMNYANG'ANYA SHAMBA LAKE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Serikali imelifuta shamba la mfanyabiashara Yusuf Manji, lenye ukubwa wa eka 714.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema leo Jumatano kuwa, shamba hilo litapangiwa matumizi mengine.


Lukuvi amesema shamba lingine la kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa eka 5,400 pia limefutwa.


Waziri amesema mashamba hayo sasa yako mikononi mwa Serikali na yatapangiwa matumizi mengine.


Lukuvi amewaonya wananchi wasivamie maeneo hayo kwa kuwa watakaokamatwa watashitakiwa.


"Muyaache maeneo hayo kama yalivyo mkijenga tutakuja kuvunja," amesema.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts