RUTI MPYA YAANZISHWA UDART | BONGOJAMII

RUTI MPYA YAANZISHWA UDART

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Udart) ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Kimara umeanzisha ruti (route) mpya kati ya Kimara na Morocco.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Udart, Deus Bugaywa amesema basi lenye namba 007 (route namba saba) litafanya kazi kuanzia saa 11:00 alfajiri hadi saa 10:00 jioni.

Amesema kuanzia saa 10:00 jioni kutakuwa na ruti mpya; namba nane na tisa (basi namba 008 na namba 009).

Bugaywa amesema basi namba 008 litaanzia Morocco na kuishia Ubungo Terminal na namba 009 litatoa huduma kati ya Ubungo Terminal na Kimara nyakati za jioni.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts