MAKUBWA YAIBUKA.... Ushindi wa Azam Fc jana waikosesha Simba mamilioni ya Mo Dewji | BONGOJAMII

MAKUBWA YAIBUKA.... Ushindi wa Azam Fc jana waikosesha Simba mamilioni ya Mo Dewji

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Shuti la ‘mwendokasi’ la umbali usiopungua mita 25 la kiungo Himid Mao limetosha kuamua matokeo ya mchezo wa Fainali ya Mapinduzi uliofanyika mjni Zanzibar.



Miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliichapa Simba bao 1-0 na kutosha kutangazwa mabingwa wapya wa Kombe la Mapinduzi.


Wakinolewa na kocha wa vijana wa Azam, Idd Cheche aliyechukua kwa muda mikoba ya Zeben Hernandez aliyetimuliwa kwa matokeo mabaya, Azam FC iliibuka na ushindi wa bao la dakika ya 13 lililofungwa na kiungo huyo wa Taifa Stars, Himid.


Ushindi huo pia umeifanya Azam FC kutwaa taji la tatu la Kombe la Mapinduzi baada ya awali kulitwaa miaka ya 2011 na 2012.


Katika mashindano hayo, beki wa Simba, Method Mwanjali amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Mapinduzi Cup, tuzo ya kipa bora imekwenda kwa Aishi Manula wa Azam FC, timu bora ya vijana ni Taifa Jang’ombe.


Mfungaji bora ni kiungo wa Yanga, Saimon Msuva, aliyeweka kimiani mabao manne, wakati mwamuzi bora wa mashindano hayo akichaguliwa kuwa Mfaume Ali.


Hata Hivyo kwa kipigo hicho ni dhahiri shari Simba watakuwa si wanakosa mamilioni ya ubingwa huo,bali pia wanakosa mamilioni yaliyokuwa yanatolewa na wafadhili wao mbalimbali ,ambao walikuwa wanatoa mamilioni hayo kama kuwapa motisha wachezaji wa Simba.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts