Wafanyabiashara ya ‘Unga’ Wabadili Mbinu,Ona wanavyofanya sasa.... | BONGOJAMII

Wafanyabiashara ya ‘Unga’ Wabadili Mbinu,Ona wanavyofanya sasa....

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamebuni mbinu mpya kwa kusafirisha na kuingiza nchini, vibashirifu (kemikali zinazotumika kutengeneza dawa ya kifua) aina ya ephedrine kisha kuvitumia kutengeneza kokeni na heroini.

Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Dawa za Kulevya, Mihayo Msikhela alisema jana kwamba wafanyabiashara hao husafirisha kemikali hizo kutoka Bara la Asia na wanapozifikisha nchini huzitumia kutengeneza dawa hizo za kulevya.

“Hivi vibashirifu aina ya ephedrine mara nyingi vinatumika kutengenezea dawa za kifua lakini hawa wafanyabiashara haramu wanabadilisha mfumo wake. Wanachofanya wanachanganya na kemikali nyingine ambazo wanatengeneza dawa aina ya heroini na kokeni,” alisema.

Pia, alisema wafanyabiashara hao hununua kemikali hizo bila kuwa na kibali cha Serikali na hudanganya kuwa zitatumika kutengeneza dawa za kifua
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts