BREAKING NEWS, RAIS MAGUFULI AAGIZA NAY WA MITEGO AACHIWE..ATAKA WIMBO HUO UBORESHWE NA UENDELEE KUCHEZWA | BONGOJAMII

BREAKING NEWS, RAIS MAGUFULI AAGIZA NAY WA MITEGO AACHIWE..ATAKA WIMBO HUO UBORESHWE NA UENDELEE KUCHEZWA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumuachia huru Rapa Emmanue Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kukamatwa juzi wilayani Mvomero mkoani Morogoro kisha kusafirishwa jana kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kwa kile kilichoelezwa kuwa wimbo wake wa WAPO alioutoa hivi karibuni hauna maadili na una maneno ya kichochezi.


Akitoa agizo la Rais Magufuli, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Rais Magufuli ametaka Nay aachiwe huru na wimbo wake aufanyie maboresho kwa kuongelea pia kuhusu wauza madawa ya kulevya na wakwepa kodi kisha uendelee kupigwa kwenye vyombo vya habari.


Aidha amesema kuwa, mara tu atakapoachiwa huru, Nay anapaswa kuonana na Waziri Mwakyembe ili ampe maelekezo yaliyotolewa na Rais Magufuli kuhusu wimbo huo.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts