GWAJIMA AZIDI KUTIKISA VYOMBO VYA HABARI, LEO KUZUNGUMZA LIVE ITV NA RADIO ONE | BONGOJAMII

GWAJIMA AZIDI KUTIKISA VYOMBO VYA HABARI, LEO KUZUNGUMZA LIVE ITV NA RADIO ONE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Bishop Josephat Gwajima amesema kuwa Ijumaa hii atatembelea IPP media kwaajili ya kuwapa pole wana tasnia ya habari kwa yaliyotokea.


Ijumaa iliyopita kituo cha Clouds kilivamiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na askari wenye mitutu kitendo kilichopingwa na wadau mbalimbali wa habari.


“Leo 24/03/2017 nitatembelea ofisi za IPP Media ikiwa ni ziara Ya kuwapa pole wanatasnia ya Habari kwa yaliyotokea,” ameandika kupitia akaunti yake ya Instagram.


Alhamisi hii Askofu huyo ametembelea EFM redio na TVE.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts