Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Tunajua kuwa alipoingia madarakani Mh Rais aliingia kwa kasi na hasira kubwa dhidi ya madudu aliyoyaona katika utawala uliopita na mara kadhaa alionekana kupinga mambo kadhaa ambayo yalionekana kuwa yamelelewa na serikali iliyopita. kauli nyingi zilitolewa na kuanza kusafisha mabaki yote ambayo aliona ni zaod la serikali iliyopita na yalikuwa na uaminifu mkubwa kule.
hali ilisababisha mambo mengi yatokee sebuleni na pia huko chumbani. na kawaida vuguvugu linalotokea chumbani huja kuonekana sebulen. kama huamini angalia mika ile wazaz wakigombana chumban wakija sebulen wataonesha tu kuna jambo hata kama watajifanya kuongea na kutabasam kinafiki.
jinamizi la lowassa liliendelea kumtesa mh rais na amesikika mara mbili huko dodoma akizungumzia suala la wa nec kuimba wana imani na lowassa. hii inaleta picha kuwa yeye hawana imani naye. asingeweza kuwafukuza wanec wote ila aliona ni bora a deal na watu kadhaa iwe onyo kwa wengine pia.
lakini ile picha ya ridhiwani na lowassa nayo ilikuwa na mchango wenye mshtuko mkubwa sana kwa waheshimiwa. na pengine ikaanza kujenga picha kuwa inawezekana kabisa kambi ya kikwete ikahamia kwa lowassa na hivyo kumpa wakati mgumu mh ndani ya ccm. hivyo solution nzuri aliona ni kurudi kwa kikwete ikiwa ni pamoja na kumpa ubunge wa kuteuliwa mama kikwete. na pia hata jana kuamua kuupa jina ukumbi ule wa ccm la kikwete ilikuwa ni katika hali ya kutengeneza urafiki ambayo haukuwah kuwepo kati yao wawili kutokana na kauli mbalimbali ambazo zimewah kuwepo hapo nyuma toka Mh alipokuwa waziri.
ameshaona siasa imekuwa ngumu ndani ya chama na kwa nchi kwa ujumla hivyo anapaswa kujiambatanisha na kundi flan. kundi hilo ameona liwe la kikwete ambaye ndiye aliyemwachia kijiti. na tutegemee mambo kadhaa pia ili kuweza kufanya urafiki huu udumu na usiwe wa mashaka kwa maana ya kuwa mama salma kuna nafasi nzuri anaandaliwa. hii familia ndiyo ambayo inaonekana haiwezi sana kuwa karibu na lowassa ingawa pia inaonesha kuwa katika siasa anything can happen. hasa kutokana na aina ya siasa za lowassa. lowassa amekuwa ni mwanasiasa anayeheshimika hata na wanaomchukia kwa kuwa na moyo dhabiti wa kutoendesha siasa za kistaarabu sana.
lowassa anaheshimika kutokana na hali yake ya kutokuwa na siasa zakishabiki na matusi kama ambavyo tumezoea watanzania wengi kuongozwa na jazba. uvumilivu wake umekuwa ni silaha kubwa dhidi ya maadui zake ambao humsema kutwa kuchwa.
jambo hili limekuwa ni kama fumbo kubwa sana ndani ya viongoz wakubwa wa ccm kiasi kwamba pale walipo wakati wote huona kma kuna kivuli cha lowassa na hii imesababisha kuwa hata anayepinga jambo lolote ndani ya chama anaonekana ni masalia ya lowassa.
kila alipozungusha macho mh kuangalia pande za kulia na kushoto mbele na nyuma alijiona amesimama peke yake na watu wengine wakiwa wapo lakini hawapo kutokna na woga kwao. aliona kuwa anapaswa kufanya mabadiliko na ili mabadiliko hayo yasimame anapaswa kuwakumbuka na kuwataka radhi watu kadhaa ambao hapo mwanzo walionekana kuwa ni wa hovyo kwake. na hivyo kuamua kuwaangukia. na gharama ya kuaangukia watu hawa itakuwa kubwa sana ili baadaye aweze jiamini na kuona amesimama.
Hayo ni Maoni ya Mmoja wa Wadau wa Siasa
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka