Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema endapo atashindwa kusimamia uhuru wa habari na vyombo vya habari nchini atajiuzulu nafasi yake kwa kuwa atakuwa ameshindwa majukumu yake katika nchi huru.
Waziri Nape Nnauye
Nape ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia na kulaani kitendo kinachodaiwa kufanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, cha kuvamia chombo cha habari cha Clauds, akiwa na askari wenye silaha na kukifananisha kitendo hicho na kuinajisi taaluma ya habari.
Waziri huyo amesema amezoea kuona matukio kama hayo yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa kwa bunduki lakini kwa nchi yetu si jambo jema kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki mkononi.
"Tumezoea kuona matukio haya yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki si sawa, kwa jambo hili tunataka kutenda haki tumsikilize Mkuu wa Mkoa ili tujue kwanini amefanya jambo hili". Alisema Nape
Kufuatia tukio hilo Waziri Nape ameunda tume yenye wajumbe takribani watano itakayoenda kumhoji Makonda na kutoa mrejesho wa kazi hiyo ndani ya masaa 24 ikiwa imeeleza sababu maalum kutokea kwa tatizo hilo.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka