SHILOLE AHAIDI KUFANYA MAKUBWA KWENYE AROBAINI 40 YA MTOTO WA NUHU MZIWANDA | BONGOJAMII

SHILOLE AHAIDI KUFANYA MAKUBWA KWENYE AROBAINI 40 YA MTOTO WA NUHU MZIWANDA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD


Shilole aka Shishi Trump ni mzungu. Amesema hana kinyongo na ex wake Nuh Mziwanda na ndio maana mwaliko wa 40 ya mtoto wa kike wa Nuh na mke wake Nawal ukihusika, ataenda kufanya makubwa.


“Mimi sinaga shobo ujue,” muimbaji huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio hivi karibuni.


“Mimi naenda kwa moyo wangu kwamba ntaenda kama msanii mwenzangu kwamba hongera kwa kupata mtoto vizawadi hivi kama vibeseni, si unajua tena mama yake mkubwa wa zamani lazima naye.. sina tatizo,” aliongeza.


Alipoulizwa kwanini hakumpa mtoto Nuh kwenye uhusiano wao, staa huyo alijibu, ‘hatukujaaliwa tu.’ Shilole amesisitiza kuwa bado yupo single kwa sasa.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts