Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewafukuza kazi mawaziri wake kadhaa akiwemo Waziri wa fedha Pravin Gordhan pamoja na naibu wake Jonas Mkabisi ambao ndio waliokua sababu kuu ya kuwepo mabadiliko haya.
Taarifa kutoka ikulu ya Afrika Kusini zinasema Malusi Gigaba ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha.
Takriban mawaziri 15 wametimuliwa katika kile kinachotajwa kama mshangao kwa serikali ya Zuma.
Aliyekuwa waziri wa fedha Pravin Gordhan

Mapema wiki hii Gordhan aliamriwa kurudi nyumbani kutoka London alipokwenda kwa ziara ya kikazi, baada ya kutuhumiwa kuwa alikua akipanga njama za kuipindua serikali iliyopo madarakani.
Maafisa kadhaa kutoka chama tawala cha ANC wanapinga kuondolewa kwa Gordhan.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka