CHANZO CHA MOTO KWENYE NYUMBA YA ZITTO CHAANIKWA HADHARANI | BONGOJAMII

CHANZO CHA MOTO KWENYE NYUMBA YA ZITTO CHAANIKWA HADHARANI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amesema kuongezeka joto katika betri za sola ndio chanzo cha moto uliounguza Nyumba ya Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe jana jioni.


Nyumba hiyo ipo mtaa wa Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga katika wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.


Amesema joto hilo limesababisha mlipuko wa moto kwenye betri za sola na hivyo nyumba kushika moto na kuteketea yote.


Polisi wanamshikilia mlinzi wa nyumba hiyo, Norbert Joseph kwa mahojiano zaidi ili kubaini kama kuna uzembe wowote uliofanywa na kusababisha moto kuwaka.


Msaidizi wa Zitto anayeifahamika kwa jina la Nyembo Mustafa ametaja thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo kwamba ni Sh 45 milioni.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts