BAADA YA MIAKA 33 MKONGWE THE UNDER TAKER ASTAAFU MIELEKA | BONGOJAMII

BAADA YA MIAKA 33 MKONGWE THE UNDER TAKER ASTAAFU MIELEKA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Sahau kuhusu City dhidi ya Arsenal na sahau kuhusu magoli 100 ya Neymar akiwa na Barceloba, usiku wa Jumapili ulikuwa usiku wa Wrestlemania.

Katika pambano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu ilikuwa kati ya Goldberg na Brock Lesnar lakini lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa zaidi ilikuwa kati ya Undertaker na Roman Reigns.

Mipambano hii ilivuta hisia za watu wengi sana, na kwa siku nyingi sana watu walitamani mipambano hii ipigwe ili kumjua nani mbabe kati ya hawa.

Na katika mechi kati ya Lesnar na Goldberg, matokeo ambayo wengi hawakuyapenda wala kuyatarajia Brock Lesnar alimpiga Goldberg na kuchukua mkanda wa Universal Champion.

Lakini mpambano mkubwa zaidi ilikuwa kati ya Roman Reigns na Undertaker, kwa muda mrefu hili lilikuwa likizungumziwa kutokana na ubora wa Reigns wengi wakiuliza atafanya nini kwa Under Taker.

Lakini katika mchezo uliokuwa mgumu sana, Reigns alionekana kummudu Taker japo kuna muda naye alielemewa na kuonekana kama atapoteza mchezo huo lakini akashinda.

Baada ya mchezo huo Undertaker alivua kofia, gloves na koti lake kuashiria ni mwisho wake kupanda ulingoni na kisha akaondoka na kuwaacha mashabiki wengi wakibubujikwa na machozi.

Under Taker ni mmoja kati ya wanamieleka bora kuwahi kutokea katika WWE akiwa ameshawahi kubeba karibia mikanda yote ya mchezo huo, huku pambano lake la kwanza ikiwa mwaka 1984 (miaka 33 iliyopita)

Kupitia kurasa zao za twitter wana mieleka wengi na mashabiki wa mchezo huo duniani walionesha hisia zao na kumshukuru Under Taker kwa kazi kubwa aliyofanya kipindi chote akiwa ulingoni.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts