HARMORAPA KWELI KIBOKO , APATA KOLABO NA MSANII TOKA ULAYA | BONGOJAMII

HARMORAPA KWELI KIBOKO , APATA KOLABO NA MSANII TOKA ULAYA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mwanamuziki Kriticos wa nchini Ubelgiji leo amewasili nchini kwa lengo la kufanya wimbo pamoja na msanii chipukizi wa Tanzania anayekuja kwa kasi sana, ajulikanae kama Harmorapa.


Mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mchana leo, mwanamuziki Kriticos ambaye anaimba miondoko ya kufokafoka ‘rap’, amesema kuwa anavutiwa na aina ya uimbaji ya Harmorapa na ndiyo sababu kuu iliyomfanya aje hapa nchini ili kufanya naye kazi.


Kwa upande wake Harmorapa anayetamba na kibao chake cha Kiboko ya Mabishoo alichomshirikisha Juma nature, amesema kuwa ujio huo kwake ni heshima kubwa na utamfanya atambulike zaidi kimataifa.


Pia amewataka mashabiki wake kukaa mlo wa kula. Ngoma hiyo itatengenezwa na kurekodiwa na mtayarishaji wa muziki, P-Funk majani.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts