KIWANDA CHA NYAMA SHINYANGA CHATAIFISHWA | BONGOJAMII

KIWANDA CHA NYAMA SHINYANGA CHATAIFISHWA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imelazimika kukitaifisha kiwanda cha nyama cha Triple S kutokana na kuendeshwa kinyume na taratibu zilizowekwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya mmiliki huyo kushindwa kukiendesha kiwanda hicho na kukiuza kinyemela kwa kampuni ya Agro Ranch ya Kagera hali ambayo imesababisha uchakavu wa majengo na mashine baada ya kutokutumika kwa zaidi ya miaka 40.

Maamuzi hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack muda mfupi baada ya kutembelea kiwanda hicho akiwa na kamati ya ulinzi na usalama na kushuhudia uchakavu wa majengo huku baadhi ya mashine zilizokuwepo katika kiwanda hicho wakati akikabidhiwa mmiliki huyo miaka kumi iliyopita zikiwa hazijulikani zilipo huku zikidhaniwa zimeuzwa kinyemela.

Akizungumza kwa niaba ya Agro Ranch Bw.Samweli Kombe amesema hajui chochote juu ya kuuzwa kwa mali za kiwanda na umiliki wa Agro Ranch kutoka Triple S huku baadhi ya nyaraka zikionyesha bado umiliki wa kiwanda ni wa mwekezaji anayeitwa Triple S.

Katika hatua nyingine Bi.Telack amewataka wananchi waliolima katika maeneo ya kiwanda kuvuna mazao yao baada ya kukomaa na kuyaachia huku akimuagiza mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wa kata ya Old Shinyanga kuhakikisha baada ya mavuno hakuna mwananchi atakayeingia katika eneo la kiwanda.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts