MAHABUSU WA KESI ZA UGAIDI WATISHIA KUGOMA | BONGOJAMII

MAHABUSU WA KESI ZA UGAIDI WATISHIA KUGOMA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Arusha. Washtakiwa 61 wanaokabiliwa na kesi 15 tofauti za ugaidi wametishia kutohudhuria mahakamani hadi upelelezi utakapakamilika.

Tishio hilo limekuja baada ya kuandika barua kwenda Ofisi ya Hakimu Mfawidhi mkoani Arusha iliyoandikwa na Yasin Sanga kwa niaba yao.

Barua hiyo inaeleza kuwa tangu mwaka 2014 walipokamatwa kesi hazijaanza kusikilizwa.

Barua hiyo ilipitia kwa Mkuu wa Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha.

Mshtakiwa Sanga katika barua hiyo yenye kumbukumbu namba 78/AR/I/VIII/184 ya Machi 30, ametaja sababu saba zilizosababisha wagome ikiwamo kuchoshwa na mambo yanayoendelea kwenye kesi hiyo.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts