Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mahakama ya katiba ya Afrika kusini imelipinga jaribio la serikali la kutaka kuweka katazo katika biashara ya pembe za faru katika matumizi ya ndani.
Matokeo yake ni kwamba pembe hizo za faru zinaweza kuuzwa ndani ya nchi huku katazo katika biashara hiyo kimataifa likiwa bado linaendelea.
Watunzaji wa wanyama pori hao wamedai kuwa, kuruhusu biashara hiyo kuendelea kufanyika kihalali kutaweza kupunguza idadi ya faru wanaouwawa kutokana na kwamba pembe za faru zinaweza kukatwa na kuacha wanyama hao hai, Hata hivyo wahifadhi wa wanyama pori hawakubaliani na hatua hiyo.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka