MAREKANI KUJENGA MTAMBO WA KUZUIA MAKOMBORA YA KOREA KASKAZINI | BONGOJAMII

MAREKANI KUJENGA MTAMBO WA KUZUIA MAKOMBORA YA KOREA KASKAZINI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Korea Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mtambo wa kisasa wa kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.


Mtambo huo wa kujilinda dhidi ya makombora, ambao hufahamika kitaalamu kama THAAD, kwa Kiingereza Terminal High Altitude Area Defense, kutokana na wasiwasi wa tishio kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imeendelea kufanyia majaribio makombora.


Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa an utakuwa tayari kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja.


Kumekuwepo na taarifa za kutokea kwa makabiliano kati ya wenyeji na polisi eneo panapojengwa mtambo huo, ambalo awali lilikuwa uwanja wa mchezo wa gofu.


Mtambo huo unajengwa katika wilaya ya Seongju


China imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.


Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.


THAAD ni nini?
Ni teknolojia ya kujilinda ya kutungua makombora ya masafa mafupi na wastani ambayo huyaharibu yanapokaribia kulipuka.
Hugonga kombora la kuliharibu
Ina uwezo wa kufika umbali wa kilomita 200 na inaweza kurushwa juu hadi kilomita 150 angani
Marekani imewahi kuweka mitambo kama hiyo Guam na Hawaii kujilinda dhidi ya uwezekano wa mashambulizi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Chanzo: BBC

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts