MSUKUMA AFUNGUKA , AELEZA SABABU ZA KUANDIKA KUWA ATAMKUMBUKA KIKWETE KWENYE GARI YAKE | BONGOJAMII

MSUKUMA AFUNGUKA , AELEZA SABABU ZA KUANDIKA KUWA ATAMKUMBUKA KIKWETE KWENYE GARI YAKE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
MBUNGE wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma, amesema kwamba maneno ‘Utakumbukwa Kikwete’ yaliyobandikwa kwenye baadhi ya mabasi yake ni ishara ya yeye kumuenzi kiongozi huyo mstaafu ambaye alimwinua kisiasa na kufikia ngazi aliyopo sasa.


Akifafanua zaidi alisema ujumbe huo unakumbusha pia mambo ya maendeleo aliyoyaanzisha kwa Watanzania na ambayo yanaendelezwa na utawala wa awamu ya tano sasa.


“Kikwete alinisaidia kuingia kwenye siasa; nimeingia katika siasa wakati wa Kikwete. Kwa hiyo nikisema tutamkumbuka ninamaanisha tutaendelea kumkumbuka kwa mema yote aliyotufanyia.”


Aidha aliongeza kwamba si basi moja tu lililoandikwa maneno hayo, kwani yapo mengine tisa yenye ujumbe huo.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts