SERENGETI BOYS WAAHIDIWA MANOTI WAKISHINDA | BONGOJAMII

SERENGETI BOYS WAAHIDIWA MANOTI WAKISHINDA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
SERENGETI BOYS
WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) watagawana fedha zote endapo watafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya vijana ya Afrika ambayo itafanyika baadaye mwezi ujao.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) litatoa zawadi ya Dola za Marekani 75,000 (sawa na Sh. milioni 157) kwa timu itakayofanikiwa kutwaa wa michuano hiyo inayoshikiliwa na Mali
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, alisema jana kuwa mbali na fedha hizo, pia yosso hao watapewa zawadi nyingine ambazo zitatangazwa hapo baadaye.

Malinzi aliongeza kuwa wanawaomba Watanzania waendelee kuisaidia timu hiyo ambayo inapeperusha bendera ya nchi kwa mara ya kwanza kwenye fainali hizo.

Naye Kocha Mkuu wa timu hiyo, Bakari Shime, alisema katika mahojiano ya si
mu kutoka Rabatt, Morocco kuwa wachezaji wanaendelea vizuri na mazoezi na lengo lao ni kutwaa ubingwa na kushiriki fainali za dunia.

Shime, kocha wa zamani wa JKT Mgambo ya jijini, Tanga alisema wanaamini hakuna kisichowezekana na wachezaji wake wako tayari kwa ajili ya kupambana.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts