Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Dar es Salaam. Shahidi wa nane katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili mshtakiwa, Salum Njwete maarufu Scorpion, Deus Magosa (45) ameieleza Mahakama kuwa maelezo aliyosomewa kortini alilazimishwa kuyatoa polisi.
“Nakumbuka nilitoa maelezo lakini si hayo kwani nilihojiwa mara mbili, kuna karatasi mbili ile ya kwanza ndiyo nilisema ukweli ambayo haipo hapa mahakamani na ya pili nililazimishwa nikubali kwamba Njwete amemjeruhi mtu kwa kumtoa macho,” alidai.
Magosa maarufu ‘Pamba D’ alidai hayo jana wakati akitoa ushahidi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.
Shahidi huyo, ambaye ni kamanda mkuu wa ulinzi shirikishi katika eneo la Buguruni na mfanyabiashara wa meza za mchezo wa pool na bodaboda, akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga, mbele ya Hakimu Mkazi Flora Haule, alidai anamfahamu Njwete kama mmoja wa walinzi katika eneo ilipo baa ya Kimboka.
Alidai alikuwa anawalinda wafanyabiashara wadogo wanaouza bidhaa kando ya Barabara ya Mandela, nje ya baa ya Kimboka na kwamba, yeye ndiye aliyemwezesha kupata kazi ya ulinzi kwa ujira wa Sh10,000 kwa siku.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka